16 Septemba 2025 - 16:35
"|Leo, yeyote ambaye hayuko pamoja na watu wa Gaza, basi hayuko pamoja na Mungu pia"

Kiongozi wa Baraza la Umoja wa Waislamu wa Pakistan, akisisitiza kuwa Marekani na Israel si wa kuaminika wala si marafiki wa Waislamu, aliongeza: Leo, yeyote ambaye hayuko upande wa watu wa Gaza, basi hayuko upande wa Mungu pia.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-: Seneta Naser Abbas Jafari, Rais wa Baraza la Umoja wa Waislamu wa Pakistan, katika mkutano wa “Mapenzi kwa Mtume Muhammad (s.a.w.W)”, alisema:

"Leo, ubinadamu wote uko chini ya shinikizo la dhulma na uonevu, na umekuwa mhanga wa utamaduni wa kifashisti na wa kinyama wa Magharibi."

Akaongeza: "Magharibi, kwa kutumia kauli mbiu ya maendeleo na ustawi, imewadanganya watu wa dunia. Lakini inapofikia kutukanwa kwa Mtume wa Mwisho (s.a.w), sura ya kweli ya utamaduni wake - yaani, ya uchi na isiyo ya kimaadili - hujitokeza wazi."

Seneta Raja Abbas alitaja hali ya Gaza kama mfano dhahiri wa ukatili wa Magharibi na akasisitiza kuwa:

"Marekani na Israel si wa kuaminika, wala si marafiki wa Waislamu; bali ni maadui wao. Utamaduni wao umejaa dharau kwa ubinadamu, hofu, usaliti, na kutoheshimu thamani za kibinadamu. Leo, yeyote ambaye hayuko upande wa watu wa Gaza, basi hayuko upande wa Mungu pia."

Pia alizungumzia shambulizi la utawala wa Kizayuni dhidi ya Qatar, akisema:

"Marekani ilihusika moja kwa moja katika shambulizi hilo, licha ya kwamba Qatar ilikuwa imempa Trump ndege yenye thamani ya dola milioni 400. Hata hivyo, viongozi wa muqawama (mapambano ya ukombozi) waliuawa shahidi."

Katika sehemu ya mwisho ya hotuba yake, Raja Naser alielezea masikitiko yake kuhusu hali ya watu walioathiriwa na mafuriko ya hivi karibuni nchini Pakistan, akisema:

"Katika mafuriko haya, ndoto na matumaini ya watu yalisombwa, watu wanyonge na wasio na msaada waliwekwa katika hatari kubwa. Lakini kwa sababu ya uzembe na uongozi mbovu wa serikali, hakuna aliyejali hali yao."

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha